November 18, 2015


Vyama vinavyounda Ukawa wamemuandikia barua Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai kutaka kujua uhalali wa Rais John Magufuli kuhutubia Bunge bila matokeo Rais wa Zanzibar kujulikana.
Wamesema hawatakubali Katiba ivunjwe kwa kumruhusu Dk Shein kuingia bungeni wakati muda wake wa kushika madaraka umeishapita tangu November 2,2015.
Uamuzi huo umetangazwa na Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe kwenye mkutano wa waandishi wa habari bungeni baada ya kikao cha wabunge wote wanaounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa).



0 comments:

Post a Comment