April 21, 2016

Baraza la Tiba asili na tiba mbadala limeyafungia maduka sita yanayouza dawa za miti shamba baada ya kubainika kuwa hayajafanya usajili kwa kipindi kikubwa pamoja na kukiuka taratibu za baraza hilo.
Hayo yamebainika kufuatia kufanyika ziara ya kushtukiza katika maeneno mbali mbali ya Mjini Magharibi na kugundua kuwa baadhi ya wamiliki wa maduka ya dawa za miti shamba  hawafuati taratibu zinazotakiwa katika uuzaji wa dawa zao.
Mrajis wa Baraza hilo Haji Juma Kundi amesema katika ukaguzi walioufanya jumla ya maduka ya dawa za tiba asili 16 na clinic tatu walizikagua na kugundua kasoro mbali mbali ikiwemo uchafu pamoja na kutokuwa na mpangilio mzuri wa dawa hizo.
Amesema kuna baadhi ya maduka ya tiba asili wamiliki wao hawajafunga  mikataba kwa kipindi cha miaka mitano ya kuendesha biashara zao jambo ambalo ni kinyume na taratibu za baraza hilo.
Kwa upande wa Cliniki zilizokaguliwa kumeonekana na changamoto kadhaa zinazohatarisha afya za wanaokwenda kupata huduma hizo ikiwemo kliniki Madawa Herbalist iliyopo maeneo ya Kijichi ambayo majengo yake yanahitaji kufanyiwa marekebisho ili kuweza kukidhi haja za wananchi.
Amesema changamoto nyengine ni kutokuwa na mpango mzuri wa kuweka dawa zao, uchafu pamoja na kutokuwa wataalamu wa kuendesha baadhi ya  kliniki hizo.
Amewataka wamiliki wa cliniki za tiba asili na tiba mbadala pamoja na wenye maduka ya tiba asili waganga pamoja na wenye vilinge kujisajili katika baraza lao sambamba na kuchunguzwa dawa zao kwa Bodi ya chakula Dawa na Vipodozi ili waweze kuwahudumia wananchi kwa uhakika na kuepusha matatizo ya kiafya.



Mmiliki wa kliniki ya ‘Madawa Herbal Clinic’ ya Bububu Kijichi
Moh’d Said Ali akitoa maelezo kuhusu huduma anazotoa  katika
kliniki yake baada ya wajumbe kutoka  Baraza la Tiba Asili na
Tiba Mbadala kufika katika kliniki yake  kufuatilia shutma za
kulaza wagonjwa  kitu ambacho kinakatazwa, wa mwanzo (kulia)
Mrajis wa Tiba asili Zanzibar Haji Juma Kundi.


0 comments:

Post a Comment