November 18, 2015

NAIBU Katibu Mkuu Wizara ya Wizara Miundombinu na 
Mawasiliano Zanzibar Tahir Abdalla akizuwiya wafanyakazi wa
 kampuni ya Simu ya Hallo tell.

kisiwani Pemba na kukuta baadhi ya wafanyakazi wa kampuni hiyo wakichimba mashimo ya kusimamisha nguzo karibu na barabara.
Naibu Katibu Mkuu Wizara hiyo Tahir abdalla amesema hakuna kipengele chochote kinachoiruhusu kampuni yoyote kusimamisha nguzo karibu na barabara hivyo kampuni ya Hallo tell ilikwenda kinyume taratibu.
 Hivyo amesema wameamua kuisimaisha shughuli hizo hadi wakuu wa kamapuni hiyo watakapokutana na uongozi wa wizara Pemba ili kujadili tena taratibu hizo.
Akitoa maelezo Afisa mdhamini wa Wizara Miundombinu na Mawasiliano Pemba Hamad Ahmed Baucha amesema mkataba wa kampuni hiyo iliyoingia na Serikali unaitaka kampuni hiyo kuwa na mtu kutoka idara ya mawasiliano pamoja na wa kitendo cha barabara (UUB) lakini kampini ya Hallotell haikufanya hivyo.
Watendaji wa Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano Pemba, kulia ni Afisa mdhamini wa Wizara hiyo Hamad Ahmed Baucha mwenye karatasi, kushoto ni Injia mkaazi wa Wizara hiyo Khamis Massoud akiwaonyesha kitu, wakikagua moja ya mikataba ya kmpuni ya simu ya Hallo Tell  baada ya kusimamisha kazi ya uchimbaji wa mashimo kwa ajili ya uwekaji wa nguzo.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)

0 comments:

Post a Comment