November 18, 2015


 MWENYEKITI wa kamati ya Mafaa Kisiwani Pemba, ambaye pia ni
Mkuu wa Mkoa wa kusini Pemba Mwanajuma Majid Abdalla, akifungua
 kikao cha dharura cha kukabiliana na maafa juu ya hali ya
Ugonjwa wa kipindupindu uliojitokeza Kisiwa Cha kojani.
Jumla ya wagonjwa 135 wameripotiwa tangu kuibuka Ugonjwa wa kipindupindu uliojitokeza katika Kisiwa Cha kojani Pemba ambapo hakuna mgonjwa aliyepoteza maisha.
Sababu kuu ya kuibuka kwa ugonjwa huo kisiwani humo kunadaiwa kunasababishwa na wananchi kutozingatia usafi pamoja na kutofuata taratibu za kiafya.
Idadi hiyo imetolewa katika kikao cha dharura cha kamati ya maafa Kisiwani Pemba kilichokuwa kikijadili juu ya kukabiliana hali ya Ugonjwa wa kipindupindu uliojitokeza katika kisiwa hicho cha Kojani.
Akizungumza katika kikao hicho Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Zanzibar Dkt Mohammed Saleh Jidawi amesema ni vyema wananchi kuchukua tahadhari za kujikinga na magonjwa ya mripuko ikiwemo kipindupindu kwa kufuata ushauri wa wataalmu wa afya hasa kuweka mazingira safi.
Amefahamishwa kamba wizara imeweka mikakati madhubuti ya kukabiliana na ugonjwa wa kipindupindu ambapo dawa pamoja na wataalamu wamepelekwa kisiwani Kojani kwa ajili ya kutoa matibabu kwa waarhirika wa ugonjwa huo.

0 comments:

Post a Comment