April 16, 2014

Serikali imetakiwa kutenga bajeti maalum kwa Kamisheni ya utalii Zanzibar ili kuweza kushughulikia nyumba za  kulaza wageni zilizokuwa hazijasajiliwa (gesti bubu) zinazoendelea kuongezeka katika maeneo mbali mbali ya kiutalii Mjini na Vijijini.
Mwenyekiti wa kamisheni hiyo Dr Ahmada Hamadi Khatib amesema Zanzibar inakusanya zaidi ya Shilingi Bilioni 2  kupitia leseni za kuendesha shughuli za utalii hivyo kuendelea kwa biashara ya magesti bubu  kunahatarisha kupungua mapato ya Serikali.
Ameyataja maeneo yaliyoongezeka nyumba  hizo ni  mji Mkongwe, Nungwi, Kizimkazi na maeneo ya Paje na Jambiani mkoa wa kusini unguja.
Dr. Khatib ameongeza pia  nyumba hizo pia zinachangia kuipotezea sifa ya Zanzibar kiutalii kutokana kukosa viwango bora vya utoaji huduma ikiwemo kuhatarisha usalama na afya za  wageni za wageni.
Ameelezea muhimu wa serikali kuweka kipaumbela cha upatikanaji wa fedha hizo ili kufanya  ukaguzi wa mara kwa mara kubaini wanaoendelea kufanya biashara ya kulaza wageni kinyume cha sheria .

0 comments:

Post a Comment