November 23, 2015



Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi CCM Abdulrahman Kinana ameongoza ujumbe wa Tanzania nchini Msumbiji kuhudhuria mkutano wa Vyama vya Siasa Kusini Mwa Afrika. 
Mkutano huo uliohudhuriwa na baadhi ya Wenyeviti na Makatibu Wakuu wa vyama  hivyo, umemalizika mwishoni mwa wiki mjini Maputo.
Mkutano huo uliofanyika wiki iliyopita ulijadili masuala ya kutatua changamoto mbalimbali za mataifa hayo na mipango ya maendeleo kwa ujumla.
Baadhi ya viongozi wa vyama hivyo vya siasa waliohudhuria ni pamoja na Mwenyekiti wa ANC ya Afrika Kusini Rais Jacob Zuma, Mwenyekiti wa FRELIMO ya Msumbiji Rais Filipe Nyusi, Mwenyekiti wa SWAPO ya Namibia Rais Hage Geingob pamoja na Kinana na ujumbe wake akiwemo Katibu wa NEC anayeshughulikia Siasa na Mambo ya Nje Dkt. Asha-Rose Migiro pamoja na Makatibu Wakuu wa Jumuiya za CCM.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman  Kinana (kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja na  Mwenyekiti wa ANC ya Afrika Kusini  Rais Jacob Zuma (kushoto) na Mwenyekiti wa
FRELIMO ya Msumbiji
Rais Philipe Nyusi  (katikati)

0 comments:

Post a Comment