
Mkutano huo utakaofanyika hapa Zanzibar kuanzia Novemba 27 hadi
28 mwaka huu utaratibiwa na chama cha WANASHERIA Mawakili Zanzibar ZLS.
Katibu wa chama hicho Omar Said Shaaban
amesema kuwa mkutano huo unatarajiwa kuwa na washiriki 400 kutoka nchi za Tanzania,
Rwanda, Burundi, Kenya na Uganda, utafunguliwa na jaji mkuu wa Zanzibar Omar Othmani Makungu.
Ameeleza kuwa mijadala mbali mbali ya kisheria itajadiliwa
ikiwemo uwezekano wa kuifanya taaluma ya sheria kuwa kichocheo cha
biashara na uwekezaji katika nchi za nchi hizo.
Amesema mfumo huo wa kutoa huduma za kisheria unatumiwa na
jumuiya mbalimbali za kisheria duniani ili
kuwawezesha wanataaluma kuwa na uwezo wa kipato bila kuwa tegemezi kwa watu
wengine.
“Kwa kweli mkutano huo ni fursa ya pekee kwa Zanzibar kwani unaowakutanisha wataalamu waliobobea
katika masuala ya kisheria kutoka nchi hizo shiriki” alisema Said.
Kwa mujibu wa maelezo ya katibu huyo amesema kupitia
mkutano huo watajadili pia uwezekano wa mawakili wa nchi hizo kufanya kazi kwa ushirikiano
bila ya mipaka wala vikwazo vya kisheria katika nchi za Afrika Mashariki .
0 comments:
Post a Comment