November 24, 2015



Jeshi la Polisi Tanzania limesema jumla ya watuhumiwa 829 wameuawa wananchi kinyume cha sheria kuanzia Januari hadi Oktoba mwaka huu.

Idadi hiyo imeongezeka ikilinganishwa na watuhumiwa wanaoshukiwa kujihusisha na vitendo vya uhalifu 785 waliouawa kwa kipindi kama hicho katika mwaka 2014.
Msemaji wa jeshi hilo, Advera Bulimba amesema hali hiyo imechangiwa na baadhi ya wananchi kuchukua sheria mikononi kwa kuwapiga, kuwadhalilisha , kuwachoma na kuwaua.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dare es Salaam Bulimba amesmea jeshi la polisi linakemea tabia hiyo na limetangaza zawadi kwa mwananchi atakayerekodi tukio la aina hiyo na kuliripoti polisi.
Amewataka wanachi kuacha mara moja tabia hiyo iliyozoeleka kwani ni ukiukwaji mkubwa wa taratibu na sheria za nchi na ni kosa la jinai.

0 comments:

Post a Comment