Mazungumzo ya kutafuta muafaka wa mgogoro wa Uchaguzi Mkuu wa
Zanzibar, yataendelea kufanyika leo Ikulu Mjini Zanzibar leo.
Mazungumzo ya kikao hicho ambacho ni cha tatu, kitaongozwa na
Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohammed Shein.
Wajumbe wa kikao hicho ni Marais wastaafu wa Zanzibar, Dk. Salmin Amour, Amani Abeid Karume, mgombea urais wa Zanzibar kwa tiketi ya Chama cha Wananchi (CUF) ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais, Maalim Seif Sharif Hamad na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi.
Mazungumzo hayo yanasubiriwa kwa hamu kubwa na wananchi baada ya Tume ya Uchaguzi Zanzibar (Zec), kufuta matokeoi ya Uchaguzi Mkuu visiwani humu Oktoba 28, mwaka huuu na kuibua mgogoro mkubwa wa Kikatiba.

0 comments:
Post a Comment