Chama cha siasa cha wakulima Tanzania AFP kimelaani kitendo
kilichofanywa na wabunge wa upinzani chini ya mwavuli wa UKAWA kuwazomea
viongozi wa Zanzibar jambo walilodai limelitia
aibu taifa.
AFP kimesema kitendo hicho hakifai kufumbiwa macho na badala
yake kinapaswa kupingwa ikizingatiwa wabunge hao wamefanya hilo katika chombo
cha kutunga sheria.
Mwenyekiti wa chama hicho taifa Said Soud Saidi amesema
inashangaza kuona viongozi waliochaguliwa na wananchi kuwawakilisha katika
bunge hilo wanafanya mambo yasiyokuwa na maana.
Amemuomba spika kuwachukulia hatua za kisheria wabunge waliofanya
kitendo hicho kwani pia kimelipa sifa
mbaya bunge hivyo.
Aidha mwenyekiti huyo wa AFP ameipongeza hutuba
ya rais wa Tanzania Dkt John Magufuli
aliyoitoa alipokuwa akifungua bunge la 11 kwa kuonesha muelekeo mzuri wa uongozi wake unakwenda
sambamba na kauli yake ya hapa kazi tu.
0 comments:
Post a Comment