Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar, Mhe
Balozi Seif Alli Iddi anafunga mkutano Mkuu wa 12 wa Chama cha Majaji Wanawake
Tanzania (TAWJA) kwa kushirikiana na Chama cha Majaji Wanawake Duniani (IAWJ)
Arusha, Tanzania.
Majaji
Wanawake takribani 600 kutoka nchi mbalimbali duniani wakiongozwa na Jaji wa
Rufaa (Mstaafu), Rais Eusebia Munuo, wa tanzania ulifunguliwa na Rais wa
Tanzania tarehe 05 Mei, 2014 .
Mkutano
huo unajadili mada ni Haki kwa wote, kupanua wigo wa mawasiliano kati ya Majaji
Wanawake duniani ili kujenga mazingira mazuri ya utendaji kazi pamoja na
kujenga ubora na uadilifu katika utoaji haki na ukuzaji (promotion) wa Haki za
Binadamu.
Chama cha
Majaji Wanawake Duniani (IAWJ) kilichoshirikiana na (TAWJA) kiliundwa rasmi
mwaka 1991 na kina wanachama takribani 4,000 kutoka kiasi ya nchi 100 kutoka
katika kila ngazi ya Mahakama.
Mhe. Jakaya Mrisho
Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Washiriki wa Mkutano wa Majaji Wanawake Duniani, Mara baada ya kufungua mkutano huo |
0 comments:
Post a Comment