![]() |
Asha Abdi Afisa utetezi TAMWA Zanzibar |
Jamii imetakiwa kutokuwaonea huruma wanafanya vitendo vya ubakaji
badala yake kuwafikisha katika vyombo vya sheria ili kuchukuliwa hatua kali dhidi
yao.
Afisa utetezi wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake
Tanzania (TAMWA) Zanzibar Asha Abdi amesema vitendo hivyo havipaswi kunyamzaiwa
kwa vile vinaweza kumuathiri alifanyiwa kitendo hicho kiafya na kiakili hata ni
kinyume na haki za msingi.
Ametoa kauli hiyo kufuatia matokeo ya hivi karibuni ya
ubakaji yaliyoripotiwa kutoka Mkoa wa Kaskazini Unguja likiwemo la kubakwa kwa
mfanyakazi wa hoteli ya kitalii ya Melia, la mtoto wa miaka 12 huko Mahonda pamoja
na lile la kumwagiwa maji ya moto mfanyakazi wa ndani huko Kwamtipura, Wilaya
ya Mjini.
Afisa Asha amesema kesi ya ubakaji katika hoteli
ya Melia ambayo mtuhumiwa ni Mkuu wa kitengo cha ulinzi katika hoteli hiyo amemuomba
radhi mhusika kufuatia kesi hiyo kuripotiwa polisi.
Tamwa imetoa pole kwa wahusika wote walofikwa
na matukio ya ukatili na kuiomba Serikali kuweka utaratibu mzuri wa kuchukuliwa
hatua za washukiwa ili kukomesha vitendo hivyo.
0 comments:
Post a Comment