Taasisi za Serikali na zisizo za kiserikali
Pemba zimetakiwa kushirikiana katika kuwaelimisha wananchi athari za mabadiliko
ya tabia nchi zilizoanza kuithiri Zanzibar.
Afisa Mazingira
wa kitengo cha kukabiliana na madiliko tabia nchi Salum Hamad Bakar amesema
ushirikiano huo ni muhimu katika kusaidia wananchi kufahamu athari za mabadiliko
hayo yanapotokea.
Akizungumza
katika majailiano ya kuwasilisha makakati wa mawasiliano kuhusu mabadiliko ya
tabia nchi Zanzibar kwa viongozi wa taasisi mbali mbali kisiwani Pemba
amefahamisha kuwa maeneo kadhaa ya kilimo na kiuchumi katika ukanda wa pwani
yameathirika na mabadiliko hayo hivyo juhudi zaidi zinahitajika kusambaza
uelewa kwa jamii.
Zaidi ya maeneo
160 ya zanzibar yameripotiwa kuvamiwa na maji ya bahari kutokana na kuongeza
kina chake kulikochangiwa na athari za mabadiliko hayo.
Akiwasilisha
maada hiyo Ruzika Niyo Muheto amesema sera ya mazingira imeainisha maeneo mbali
mbali yaliyovamiwa na maji ya chumvi hali inayotilia shaka hatma ya maisha yao
na kusisitiza umuhimu wa sekta zote za Serikali na Binafsi kutekeleza mkakati
huo kwa maslahi ya taifa.
Nae Afisa Idara
ya kilimo Pemba Idrisa Hassan Abdalla ameitaka kuelezwa kwa kina sababu
zinazopeleka suala la mabadiliko ya tabia ya nchi ili wananchi wafahamu athari
zake na kuchukuwa hatua.
0 comments:
Post a Comment