Waislamu
mbalimbali nchini wametakiwa kutoa michango yao ili kufanikisha ijitimai ya
kimataifa inayotarajiwa kuanza juni 16 mwaka huu.
Ijitimai
hiyo inafanyika kila mwaka kwa karibu miaka 20 sasa ikiwa na lengo la
kuwakumbusha waumini wa dini hiyo juu ya
mambo mema.
Naibu wa jumuiya
ya Fiisabillahi Tablighi Markaz Zanzibar Sheikh Wakati Hassan amesema tayari
maandalizi yameanza kwa ajili ya ijitimai hiyo ikiwemo ujenzi wa baadhi ya
sehemu mbali ikiwemo vyumba na vyoo.
Amefahamisha
kuwa ijitimai hiyo itahudhuriwa na waislamu kutoka nchi za Uganda, Afrika ya kusini,
Malawi, Zambia, Kenya, Rwanda na Tanzania bara.
0 comments:
Post a Comment