![]() |
Kamishna wa Elimu Zanzibar Maryam Abdalla Yussuf |
Amesema utafiti
wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar umegundua sababu
mbali mbali zinazochangia wanafunzi kutoroka skuli ikiwemo tabia ya baadhi ya
wazazi kutowapatia mahitaji muhimu ya kimasomo watoto wao.
Akizungumza
katika uzinduzi wa mradi wa kuhamasisha kupunguza wimbi la utoro maskulini wa
jumuiya ya kuwanasua vijana na watoto katika matatizo yanayowakabili (zao) Kamishna
Maryam amesema iwapo umuhimu wa elimu utahamasishwa zaidi kwa wanafunzi
utapunguza tatizo hilo la utoro.
Amefahamisha
tabia ya vijana kuacha masomo kunaongeza idadi ya watoto wasiojua kusoma na
kuandika kunapunguza idadi ya wasomi wanaohitajika kwa maendeleo ya Zanzibar.
Amewataka walimu
na wazazi kufuatilia kwa karibu maendeleo ya watoto wao kwani nimiongoni mwa
jukumu lao muhimu katika kuwandaa kimasomo watoto wao.
![]() |
wanafunzi zanzibar |
Fatma Bakari
Makame akisoma risala amesema jumuiya hiyo imelenga kuelimisha vijana
juu ya athari za maambukizi ya virusi vya ukimwi kwa wanafunzi pamoja na kupiga
vita mimba za umri mdogo na imefanikiwa kuwarudisha wanafunzi kuendelea
na masomo katika skuli za Mtopepo A, Kilimahewa, Mwembe Makumbi na wengine
wamepelekwa katika Kituo cha Elimu mbadala.
0 comments:
Post a Comment