
Viongozi
hao akiwemo mpiga picha wa Shirika la Utangazaji la TBC, George Kasembe wamepatiwa
matibabu kwa majeraha waliyoyapata na wameendelea na ziara yao ya kuangalia
athari za mvua..
Kiasi ya watu
10 wakiwemo watoto wadogo wameripotiwa kupoteza maisha kutokana na mvua
zinazoendelea kunyesha katika jiji la dar es salaam pamoja na kusababisha
uharibifu mkubwa wa mali na miundombinu ya madaraja na nyumba za makaazi.
Kamanda wa kanda
maalum Dar es salaam Suleiman Kova mapema
aliarifu kuwa hali sio nzuri jijini
humo na
kuwataka wananchi kuchukuwa tahadhari
kwenye makazi yao na kupunguza mizunguko isiyo ya lazima kutokana na njia nyingi kuwa
na mashimo.

0 comments:
Post a Comment