April 30, 2014

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein ameipongeza Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais kwa kukamilisha utafiti wa ufikiaji wa huduma kwa watu wenye ulemavu .
Amesema matokeo ya utafiti huo yamekuwa msingi wa kuandaa Sera ya Maendeleo ya Watu hao Zanzibar.
Katika kikao hicho cha kujadili wa Taarifa ya Utekelezaji wa Mpangokazi wa Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais kwa kipindi cha robo tatu ya mwaka wa fedha 2013/2014 rais Shein amehimiza suala la vipaumbele vya Wizara na Idara kwenda sambamba na majukumu ya msingi ya Wizara na Idara (core functions) husika.
Kuhusu suala la msaada wa uendeshaji wa vituo vya vijana walioacha madawa ya kulevya nchini maarufu ‘Sober Houses’ amehimiza ushiriki wa wadau wengi zaidi na Ofisi hiyo kuangalia kwa upana zaidi suala hilo ikiwemo kuandaa mpango maalum endelevu  wa msaada wa jamii na Serikali kwa vituo hivyo.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Bi Fatma Abdulhabib Fereji amesema  kipindi cha Julai 2013 hadi Machi 2014 afisi hiyo imekamilisha utafiti huo Mkakati wa Taifa wa Mabadiliko ya Tabianchi.
Amesema katika mwaka ujao wa fedha ni Sera ya Maendeleo ya Watu wenye Ulemavu, Sera ya UKIMWI, Kanuni ya Sheria ya Dawa za Kulevya, Mkakati wa Kudhibiti Taka Ngumu na Mpango wa Utekelezaji wa Mabadiliko ya Tabianchi. 

0 comments:

Post a Comment