April 29, 2014

Waziri wa habari utamaduni utalii na michezo Zanzibar Said Ali Mbarouk amesema bado Marekeni haijatumia fursa za utalii wa  Zanzibar.
Amesema licha ya kupiga hatua katika sekta hiyo idadi ya  raia wa nchi hiyo hasa katika utalii wa daraja la kwanza ni kiwango kidogo ikilinganishwa na  wageni wanaotembelea Zanzibar.
Alikuwa akizungumza na ujumbe wa Shirika la utangazaji la Marekani (VOA) ukiongozwa na mtangazaji Dk Shaka Salli unaoangalia namna Zanzibar ilivyofaidika  katika  miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
Waziri Mbarouk amemshauri mtangazaji huyo kusaidia kutangaza na kushawishi raia wa nchi hiyo kutembelea Zanzibar na Afrika.
Aidha ameliomba shirika la VOA kujenga ushirikiano na Shirika la utangazaji la Zanzibar ZBC kwa ajili ya kuwapatia mafunzo waandishi wa habari ili kuimarisha ufanisi wa kazi zao.
Nae Dk Shaka Salli amesema voa iko tayari kushirikiana na zbc katika kukuza matangazo yake na sekta ya utangazaji Zanzibar

0 comments:

Post a Comment