Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imesema
haitafumbia kufumbia macho matukio ya uchomaji moto wa nyumba unaoaminika kauwa wa
kimazingara katika kijiji cha koani kibondemaji.
Akizungumza katika ziara ya kutembelea eneo
hilo Waziri wa nchi afisi ya Makamo wa pili wa Rais Mohamed Aboud Mohamed
amesema tukio hilo limekuwa likiwakosesha watu amani na kuwaongezea umasikini.
Amesema serikali iko tayari kutumia mbinu
zozote kwa kushirikiana na wakaazi wa eneo hilo pamoja na vyombo vya ulinzi na
usalama kulipatia ufumbuzi tatizo hilo pamoja na kujua chanzo halisi cha mkasa
huo wa kushangaza.
Mh aboud ambae alishuhudia moto huo ukiwaka
katika nyumba mbili kwa wakati tofauti na amewataka wananchi kuwa wastahamilivu
kwa kuelewa kuwa huo ni mtihani unaowakabili kwa kipindi hiki.
Nyumba hizo zinazokadiriwa kufikia saba zenye
wakaazi 39 zimeanza kuchomwa moto tokea 4 April 2016 ambapo tayari wakaazi wa
nyumba hizo wameathirika baada ya mali zao kadhaa kuchomwa
moto.
Akielezea tukio hilo sheha wa Shehia ya Koani Kibondemaji
B Tunza Ali Shaali amesema moto huo umekuwa ukiwaka bila ya kutegemewa na mara
nyingi hutokea pale nyumba inapokuwa haina mtu hali inayowafanya kushindwa
kuendelea na kazi zao za kawaida.
Katika ziara hiyo Wazri aboud amewakabidhi wananchi hao walioathirika
na tatizo la kuunguliwa kwa nyumba zao vifaa mbali mbali vikiwemo magodoro,
mchele, sukari na vifaa vya nyumbani pamoja na fedha taslim kutoka Kamisheni ya
kukabiliana na Maafa Zanzibar.
Wakati huo huo Waziri Aboud mohamed amelitaka jeshi la polisi
kuhakikisha hadi Jumatatu 18 April wanatoa taarifa juu ya uchunguzi kwa watu
waliohusika na uchafuaji wa maji katika huko Bububu.
Amesema jambo hilo si la kuvumiliana na kuoneana
muhali kwa vile linawagusa watu wote na ni kinyume na ubinadamu hivyo ni lazima
kwa polisi kuchukua hatua hizo haraka.
Mh Aboud ameeleza hayo alipokuwa akizungumza
na wananchi walioathirika na uchafuzi wa maji ya zawa baada ya kutiwa mafuta
machafu (mobile mchafu) wiki iliyopita .
Amesema serikali kwa sasa haiwezi kuvumilia
vitendo hivyo kwani vitendo hivyo ambavyo vinarejesha nyuma juhudi za serikali
za kuwapatia wananchi huduma hiyo.
Pia Waziri
Aboud pia ametembelea ghala la kuhifadhia vifaa vya maafa Saateni pamoja na
kuangalia maendeleo ya ujenzi wa jengo la afisi ya Kamisheni
ya Kukabiliana na Maafa Zanzibar.
Akizungumza katika ziara hiyo Mkurugezi Mtendaji
wa Kamisheni hiyo Ali Juma Hamadiamesema jengo hilo litakuwa ni kituo kipya cha
operesheni za taasisi hizo ambayo itakuwa na ofisi pamoja na ghala lakuhifadhia
vitu mbali mbali vya maafa.
Waziri wa nchi Afisi ya Makamu wa pili wa Rais Mohamed Aboud Mohamed akiangalia moja ya kisima maji yake yaliyoathirika na mafuta hayo machafu huko Bububu nje ya Mji wa Zanzibar |
Mkurugenzi mtendaji wa Kamisheni ya Kukabiliana na Maafa Zanzibar akimtembeza Waziri Aboud kuangalia maendeleo ya ujenzi wa afisi ya taaisisi hiyo huko Maruhubi nje kidogo ya Mji wa Zanzibar |
0 comments:
Post a Comment