April 07, 2016

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Ali Mohamed Shein leo amewaongoza viongozi na wananchi mbali mbali katika kisomo maalum cha kumuombea dua Rais wa kwanza wa Zanzibar Marehemu Abeid Amani Karume kilichofanyika Afisi kuu ya CCM Kisiwandui.
Marehemu Karume alikuwa kiongozi wa chama cha Afro-Shirazi (ASP) na makamu wa kwanza wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania aliuawa tarehe 7 April, 1972 katika makao makuu ya ASP ambayo sasa ni ofisi kuu ya CCM.
Kisomo hicho kilihudhuriwa pia na Makamo wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania   Samia Suluhu Hassan aliemuwakilisha Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli

Rais mstaafu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Amani Abeid Karume pamoja na viongozi wengine na wananchi walihudhuria kisomo hicho na baadae pia   viongozi wa madhehebu mbalimbali ya dini walipata fursa za kumuombea dua marehemu Abeid Amani Karume.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein 
akiweka shada la Maua kwenye Kaburi la Rais wa kwanza wa Zanzibar na Muasisi wa ASP
 marehemu Sheikh Abeid Amani Karume wakati wa Dua maalum ya kumbukumbu
ya kifo cha Muasisi huyo  inayoadhimishwa kila mwaka
ifikapo April 07, Kisiwandui Zanzibar.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan,
 akijiandaa kuweka Shada la Maua kwenye Kaburi la Rais wa kwanza wa Zanzibar 
na Muasisi ASP marehemu  Sheikh Abeid Amani Karume wakati wa Dua 
maalum ya kumbukumbu ya kifo cha Muasisi huyo na amemuwakilisha
Rais John Magufuli ambaye yuko nje ya nchi kikazi.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan 
wa pili kulia Mama Mwanamwema Shein kulia Mama Asha Ali Iddi wa pili kushoto na
 Mama Zakia Bilal kushoto, wakiwa katika Dua ya pamoja kwa ajili ya kumuombea 
Rais wa kwanza wa Zanzibar marehemu Sheikh Abeid Amani Karume wakati wa Dua 
maalum ya kumbukumbu ya kifo cha Muasisi huyo Kisiwandui Zanzibar.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan  
akisalimiana na Rais Mstaafu wa Zanzibar Mhe. Amani Abeid Karume baada ya dua 
ya pamoja na Viongozi mbalimbali na Wananchi wa Bara na Visiwani  ya kumuombea 
Rais wa kwanza wa Zanzibar na Muasisi ASP Hayati Sheikh Abeid Amani Karume .

0 comments:

Post a Comment