Rais Magufuli
ameipongeza ofisi ya Bunge kwa kubana matumizi na kufanikiwa kuokoa shilingi
Bilioni 6, ambazo zitatumika kutengeneza madawati ya wanafunzi wa shule na
amezitaka ofisi na taasisi nyingine za serikali kuiga mfano huo.
Ameagiza fedha hizo
zipelekwe Idara ya Magereza na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) ili vyombo hivyo
vifanye kazi ya kutengeneza madawati yanayotarajiwa kuwa zaidi ya 120,000
ambayo yatasambazwa katika shule ili kukabiliana na tatizo la wanafunzi
wanaokaa chini kwa kukosa madawati.
Hundi Kifani ya fedha
hizo imekabidhiwa kwa Mheshimiwa Rais na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Akson, ambaye amesema Ofisi ya Bunge
imetekeleza wito wa serikali wa kubana matumizi ambapo kiasi hicho cha shilingi
Bilioni 6 kimepatikana kwa kipindi kifupi cha takribani nusu mwaka.
Katibu wa Bunge Dkt.
Thomas Kashilila ametaja maeneo ambayo Bunge limebana matumizi kuwa ni Safari
za nje ya nchi, Mafunzo nje ya nchi, Machapisho na ununuzi wa majarida,
Shajala, Chakula na Viburudisho, Mtandao, Malazi hotelini, Matibabu ya wabunge
na familia zao nje ya nchi, Umeme, Maji, Simu na Uendeshaji wa Mitambo.
Rais Dkt. John Pombe Magufuli
akimsikiliza Naibu Spika Dkt. Tulia Ackson kabla ya
kukabidhiwa hundi kifani
yenye thamani ya Shilingi Bilioni Sita.
|
Gerson
Msigwa
Kaimu
Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es
salaam-11 Aprili, 2016
0 comments:
Post a Comment