Tanzania inakusudia kuipa nguvu Sera ya wazee ili kuwa Sheria
itakayowasaidia wazee kujikwamua katika changamoto zinazowakabili.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, wazee na Watoto Ummy
Mwalimu amesema matayarisho ya mswaada wa Sheria hiyo ili kuiwasilisha Bungeni
mwezi Septemba.
Akizungumza na wazee wa Dare s salaam ameeleza Serikali imelenga kuhakikisha wazee wanapata mahitaji
yao muhimu ikiwemo huduma ya afya na kuwezeshwa kiuchumi ili kukabiliana na changamoto
zinzowakabili katika maisha yao ya kila siku.
Waziri ameziagiza Halmashauri zote nchini kuhakikisha Hospitali zake zinanzisha
na kuimarisha huduma za matibabu kwa wazee ili kupata kwa urahisi.
Nae Mwenyekiti wa wazee wa Mkoa wa Dar es Salaam Mzee Hemed Mkali amesema
wanaimani serikali inayoongozwa na Rais John Magufuli kuwa itawasaidia katika kutatua
changamoto zinazowakabili.
Kikao hiki cha wazee wa mkoa wa Dar es salaam na Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,wazee na Watoto dhumuni kubwa ni kwa wazee ni kuomba kukutana na Mhe. Rais Dkt John Pombe Magufuli kujadili hatma ya maendeleo ya wazee nchini.

0 comments:
Post a Comment