Matayarisho kwa ajili ya sherehe za kumuapisha
raisa mteule wa Zanzibar Dkt Ali Mohamed
Shein yamekamilika.
Mwenyekiti wa kamati ya sherehe na maadhimisho
ya kitaifa Balozi Seif Ali Iddi akiwa pamoja na makamanda wa vikosi
hivyo na baadhi ya watendaji wakuu wa Serikali walikagua hatua za mwisho
za maandalizi.
Sherehe hizo zitakazofanyika katika uwanja wa amani
mjini Zanzibar zitapambwa na vikosi vya
Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Polisi, Kikosi cha Kuzuia Magendo (KMKM),
Mafunzo, Jeshi la Kujenga Uchumi (JKU) , Valantia (KVZ) na Kikosi cha Zimamoto
na Uokozi (KZU).
Akizungumza katika ziara hiyo Balozi Seif amewaomba
kujitokeza kwa wingi katika siku hiyo
pamoja na kuwataka kuelewa kuwa uchaguzi umeisha kila mmoja
anapaswa kuhakikisha anaelekeza nguvu zake katika ujenzi wa
taifa ili kukuza uchumi wa Zanzibar.
Dr. Ali Mohammed Shein wa Chama cha
Mapinduzi CCM alishinda uchaguzi baada
ya kupata kura 299,982 sawa na
asilimia 91.4% ya kura zote zilizopigwa kwenye uchaguzi wa marudio Zanzibar uliofanyika jumapili ya Machi 20,2016.
0 comments:
Post a Comment