Uwanja
wa pemba unatarajiwa kuanza kutoa huduma za kuruka na kutua ndege nyakati
zote hivi karibuni
Hii
ni kufuatia kukamilika mradi wa uwekaji taa katika njia za kupitia ndege uliogarimu kiasi cha shilingi
bilioni 1.5
Fundi
wa Mamlaka ya viwanja vya ndege Zanzibar Mzee Abdalla amesema uwanja huo kwa sasa utakuwa na uwezo wa kutoa
huduma hadi usiku na mchana tofauti na ilivyokuwa awali zinaishia saa kumi na
mbili za jioni.
Amesema
tayari majaribio ya awali ya taa hizo
yamefanyika na sasa wanaendelea na kazi za kubadilisha miundo mbinu ya mfumo
wa umeme na kuweka wa kisasa uwanjani hapo.
Funfi
Aballa amefahamisha kuwa mfumo huo utaweka mtandao wa pamoja wa umeme ambapo
pia wataweka jenereta litakalosadia kuendelea na kazi inapotokea hitilafu ya
umeme.
Uwakaji
wa taa hizo unafanyikwa chini ya kampuni moja kutoka Ujerumani ya Sage Gate awali
ulitarajiwa kumalizika mwezi Septemba mwaka huu.
0 comments:
Post a Comment