Aliyekuwa Spika wa Bunge la Kumi,
Anne Makinda amesema hatagombea tena nafasi ya Uspika wa Bunge la 11 la
tanzania.
Mama Makinda amesema
kuwa hanampango wa kugombea tena nafasi hiyo na wala hajachukua fomu kama
inavyo elezwa na baadhi ya watu.
Hata hivyo, hadi pazia la kuchukua
na kurudisha fomu za kuwania Uspika wa Bunge la 11 la Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania linafungwa, Mama Anna Makinda alikuwa hajarudisha fomu yake hivyo
kuonesha dhahiri kuwa ameachana na mpango huo.
Aliyekuwa Spika wa Bunge la Kumi, la Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Anne Makinda ametangaza kutogombea nafasi ya Uspika wa
Bunge baada ya kuliongoza Bunge hilo kwa kipindi cha miaka mitano.
akizingumza na waandishi wa
habari katika ofisi za Bunge jijini Dar es Salaam Makinda amesema ameona wakati
umewadia wa kuwaachia wengine kusika wadhifa huo katika Mhimili huo
muhimu wa Serikali.
Ameongeza kuwa ametumikia nafasi
mbalimbali katika Siasa kwa kipindi cha miaka 40 ndani ya Bunge, ikiwemo nafasi
ya Waziri ,Mwenyekiti wa Bunge,Naibu Spika na Spika hivyo kwa sasa
ameamua kung’atuka katika masuala ya uongozi.
“Kama yalivyo matakwa ya
kisheria na demokrasia ya hapa nchini wanasiasa wanatumikia nafasi zao
mbalimbali kwa kipindi cha miaka mitano na kisha wanarudi kuomba tena ridhaa
kwa wananchi kuongoza”,alisema Mhe.Makinda.
Hata hivyo Mheshimiwa Spika
amewaambia waandishi wa habari kuwa katika kipindi cha uongozi wake, Bunge
lilifanyakazi kwa ushirikiano na liliweza kuisimamia Serikali hadi kupelekea
baadhi ya Mawaziri kujiuzulu.
Ameongeza kuwa Bunge la 10
lilifanikiwa kubadilisha mfumo wa bajeti kwa kuweka sheria mpya za bajeti
ambayo iliongeza nidhamu katika matumizi ya fedha.
Teyari Makada 21 wa CCM
wamejitokeza kuwania nafasi ya Uspika wa Bunge akiwemo Dkt. Emmanuel Nchimbi,
Samwel Sitta, Dkt Didas Masaburi, Balozi Philip Marmo, , Job Ndugai, Abdallah
Mwinyi na Mussa Hassan ‘Zungu’ anaewania unaibu spika ni miongoni mwa majina ya
makada wa CCM waliojitokeza kuwania nafasi hiyo.
0 comments:
Post a Comment