November 27, 2015


Jaji mkuu wa Zanzibar Omar Othman Makungu amewataka wanasheria kuingia katika ushindani wa kibiashara na uwekezaji wa fani hiyo huku wakizingatia kuendelea kutoa huduma bora za kisheria kwa wananchi wa kipato cha chini.
 Amesema mabadiliko hayo ya kitaaluma iwapo yatazingazitia hali halisi ya wananchi wa kipato cha chini na kwa kutumia wanasheria wazalendo badala ya wageni kwa lengo la kuongeza kipato cha nchi.
Rai hiyo ameitoa wakati akifungua mkutano mkuu wa Jumuiya ya wanasheria mawakili wan chi za Afiraka Mashariki uliofanyika katika Hoteli ya Sea Cliff huko Mkoa wa Kaskazini Unguja.
Amewashauri kuweka msisitizo wa kukemea tabia ya wawekezaji wa kimataifa wanaofungua makampuni makubwa ya kibiashara katika nchi za Afrika Mashariki wanao watumia wanasheria kutoka nchi za kigeni na kuwakosesha fursa wanasheria wazalendo wenye uzoefu huo.
Nae Rais wa Jumuiya ya wanasheria mawakili ya Afrika Mashariki, Nassor Khamis Mohamed amesema mkutano huo licha ya kujadili suala la uwekezaji kupitia fani ya sheria pia watajadili namna ya kuweka mazingira ya nchi za Afrika Mashariki ikiwemo Tanzania Bara, Zanzibar, Kenya, Rwanda, Burudi, Rwanda, Uganda zinaendelea kuwa  salama kwa  msaada wa kisheria.
Baadhi ya Washiriki kutoka sehemu mbalimbali wakifuatilia mkutano huo.



Baadhi ya Washiriki wa Mkutano huo wa Kimataifa wa 20 wa Wanasheria wa Afrika Mashariki wakiwa katika Ukumbi wa Mkutano.

0 comments:

Post a Comment