Wizara ya uwezeshaji, ustawi wa jamii,
vijana, wanawake na watoto umeandaa mfumo wa ufuatiliaji na tathmini masuala ya
haki za mtoto Zanzibar.
Mpango huo unalenga kufahamu namna ya kutekeleza na
kusimamia haki za kundi hilo nchini ili
kupata taarifa sahihi na kwa wakati.
Mkuregenzi mipango, sera, na utafiti wa Mhaza Gharib Juma akizungumza na maafisa wa
mipango na takwimu wa taasisi zinazotekeleza mkakati wa haki za watoto
ameelezea umuhimu wa mfumo huo katika
kusimamia na kuandaa mipango bora.
Amesema
inaamini kuwa mpango huo utakuwa nyenzo
nzuri ya kufahamu changamoto ziliopo na kuwa na njia mbadala za kupunguza tatizo hilo sambamba
na Mpango wa kukuza uchumi na kuondoa umasikini
Zanzibar (MKUZA).
Mkutano huo
umewashirikisha maafisa kutoka
jeshi la polisi,Mahakama,DPP,Chuo cha mafunzo na Unicef umetayarishwa kwa
ufadhili wa jumuia ya ulaya.
0 comments:
Post a Comment