May 09, 2014

Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
 akihutubia Kongamano la Kampeni ya
kukomesha mauaji dhidi ya Tembo.
Makamo wa Rais wa Tanzania Dkt.Ghalib Bilali amesma kuwa serikali kwa kushirikiana na jumuiya ya kimataifa, inafanya mikakati mathubuti ya kukabiliana na ujangili wa wanyamapori kwa kuwabainisha majina wale wote wanaojihusisha na biashahara haram ya pembe za ndovu.
Akifungua mkutano huo wa siku 4 kupinga ujangili dhidi ya tembo uliongezeka mbali na kupigwa  marufuku ametaja kuwa serikali sasa itaweka sheria kali ya kutoa adhabu kali kwa watakaobainika wanajihusisha na biashara haramu ya meno ya tembo ndani na nje ya nchi.
Waziri wa maliasili na utalii Lazaro Nyalandu   amesema wizara imeomba serikali kuajiri haraka  askari wa wanyama pori wapatao 430 hadi mwezi wa saba mwaka huu kufanya kazi katika mbuga zote za wanyamapori nchini..
Amefafanua kuwa pia serikali imeagiza helkopita 3 aina nchini marekani kwa ajili ya kupambana na majagili wanaoua tembo na kusafiri pembe za ndovu kwenda mataifa mengine.



Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa Kongamano hilo, baada ya kufungua rasmi leo kwenye Hoteli ya Hyat Kilimanjaro, jijini Dar es Salaam

0 comments:

Post a Comment