May 08, 2014


Mamlaka ya usafiri baharini Zanzibar imelamikia Idara ya uhamiaji Tawi la Mtwara kwa kitendo cha kuwakamata mabaharia wa meli ya mizigo katika eneo hilo iliyosajiliwa Zanzibar.
Mkurugenzi wa mamlaka hiyo Abdi Omar Maalim amesema kitendo hicho ni cha uonevu kwani meli hiyo  inaruhusiwa kufanyakazi ndani ya Tanzania kwa mujibu wa sheria za usafiri wa baharini.
Ameeleza mabaharia hao raia wa Kenya wamekamatwa kwa madai ya kukosa kibali cha kazi, wakati wanaruhusika wakiwa na utambulisho wa uraia na kibali cha usajili wa meli.
 Amefahamisha kuwa kuna mabaharia wengi wa Tanzania wanaofanya kazi kenya bila ya kibali cha kazi hivyo ni vyema idara ya uhamiaji kuwa makini kwa kufuata sheria na kanuni za nchi.
 Amesema maamuzi yaliyofanywa na idara ya uhamiaji mtwara kutaka kuwashtaki mabaharia hao ni kitendo cha ubaguzi kwani kinaweza kusababisha mgogoro baina ya tanzania na nchi nyengine wananchama wa jumuiya ya Afrika Mashariki

0 comments:

Post a Comment