Jumla ya wanawake 200 na wanaume
21 wameripotiwa kufanyiwa vittendo ya ukatili wa kijinsia katika kituo cha mkono
kwa mkono Chake chake Pemba, ambapo wengi wao wakiwa watoto, ikiwa ni pamoja na
kesi 92 za ubakaji, kuanzia mwezi Julai hadi disemba mwaka jana.
Kesi nyengine
zilizoripotiwa kituoni hapo kwa kipindi hicho ni kesi 15 za kulawiti, ambapo
wanawake walikuwa watatu na wanaume walikuwa 12, huku kesi za zilikuwa 58
zikimuhusisha mtoto mmoja wa kiume.
Akizungumza na mwandishi wa
habari hizi afisini kwake mjini Chakechake, Mratibu wa kituo hicho Fatma
Abdalla, alisema pia walipokea kesi 17 za shambulio la mwili ambapo wanawake
walikuwa 15 na wanaume wawili.
Aidha alifafanua kuwa kesi
nyengine zilizopokelewa ni shambulio la aibu ambapo kesi hizo kwa kipindi cha
mwezi Julai mwaka jana hadi disemba mwaka 2013 zilipokelewa kesi 13 ambapo
wanaume walioofanyia tendo hilo walikua sita na wanawake saba.
“Kwakweli kituo hichi tokea
kilipofunguliwa mwezi wa saba mwaka 2012 tumekuwa tukipokea wastani wa kesi 12
kwa mwezi za aina mbali mbali za ukatili wa kijinsia kwa wanawake na
watoto’’,alifafanua Mratibu huyo.
Aidha alieleza kuwa
miongoni mwa sababu ya kujitokeza kwa matendo hayo ni kuporomoka kwa maadili
ndani ya jamii usuluhishaji wa kesi hizo
nje ya mahakama .
Amefahamisha kuwa
ilikupunguza vitendo hayo ni kwa jamii inapaswa kuacha tabia ya hizo na
kusimamia uslama wa watoto wao.
0 comments:
Post a Comment