April 27, 2014

 Watanzania 12 wametiwa mbaroni nchini Madagascar wakituhumiwa kukutwa na meli iliyosheheni magogo ya miti adimu na ghali ambayo yamepigwa marufuku kuvunwa humo.
Shirika la Habari la Ufaransa (AFP), limesema Watanzania hao wanashikiliwa tangu wiki iliyopita na meli hiyo iliyosajiliwa kusajiliwa Tanzania ilikutwa katika ufukwe wa Madagascar baada ya kupata hitilafu ikiwa imesheheni magogo 2,135 aina ya rosewood yayokatazwa kuvunwa au kusafirishwa nchini humo.

Baadhi ya wanafamilia wa mabaharia hao wamesema ndugu zao wanashikiliwa ni ndugu zao na meli hiyo inaitwa Mv Wete na mmiliki wake Said Abdulrahman Juma jina la umaarufu Saidi Mbuzi na hadi sasa hawajakutana nae kwa ajili ya kupata taarifa zaidi.

wananchi hao wamedai kuwa wamekuwa wanawasiliana na ndugu zao walikuwa ndani ya meli waliokamatwa Madagascar tangu March 29 2014 waliwaambia kuwa wanatakiwa kulipa shilingi milioni 17 ili kuachiwa huru.

Mabaharia ni Amour Ali Juma ambae ni Nahodha, Revinda Jeram Harua, Mohamed Amir Mohammed, Khatib Salum Bakar, Omar Hassan Mwalim, Mussa Yussuf Mussa na Ali Amour Ali.

Wengine ni Eduward Felis Visso, Haji Ali Haji, Yussuf Ayoub Rashid, Mbarouk Bakar Khamis na Salum Khamis Hassan.

Mkurugenzi wa Mamlaka ya usafiri baharini Zanzibar Abdi Omar amesema mmiliki wa meli hiyo amewasiliana na wizara ya mambo ya nje kupitia balozi wa Tanzania nchini Msumbiji ili kuchukuwa taratibu kwa mabaharia hao.

Hata hivyo Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Uhusiano wa Kimataifa,Michael Haule amearifu kuwa Serikali Tanzania bado haijapata taarifa kuhusu mabaharia hao wa Watanzania waliokamatwa pamoja na meli yao huku jeshi la polisi likiendelea kufuatilia taarifa hiyo.

Mwaka 2009 serikali ya Madascar ilipiga marufuku uvunaji wa magogo ya mti wa mwaridi -rosewood unaotumika kutengeneza samani na zinakuwa na thamani kubwa.

0 comments:

Post a Comment