Makamu
wa kwanza wa Rrais wa Zanzibar Maalim Seif
Sharif Hamad amesema taasisi binafsi
zinazosimamia kuwaendeleza watoto yatima zinasaidia serikali kupunguza mzigo wa
kuwapatia huduma muhimu wananchi.
Amesema
mbali na unafuu huo jamii pia ina wajibu wa kuunga mkono kusaidia yatima
ili waweze kupata mahitaji yao ya
kibinaadamu.
Amesema
katika juhudi hizo wanawajibu wa kuziunga mkono jumuiya na taasisi nyengine
zenye jukumu la kusimamia mayatima kwa
kutoa misaada mbali mbali kwa maendeleo ya watoto hao
Maalim
seif ameeleza hayo katika hotuba iliyosomwa na katibu mkuu wizara ya nchi afisi
ya makamu wa rais dr omar dadi shajak katika sherehe za kuadhimisha siku ya
watoto yatima iliyoandaliwa na taasisi ya muzdalifah huko jozani mkoa wa
kusini.
Ameiomba
taasisi hiyo kuhakikisha watoto wanaowasimamia wanaendelea kupata elimu
itakayowakuza katika maadili mema.
Nae katibu mtendaji wa
jumuiya ya Iistiqama Farouk Hamad amesema taasisi hiyo imeshatoa misaada mbali
mbali ikiwemo ujenzi wa misikiti na madarassa pamoja na uchimbaji wa visima 40
vya maji maeneo ya zanzibar kwa lengo la kuwapunguzia wananchi uhaba wa huduma
hiyo muhimu.
0 comments:
Post a Comment