Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano
wa Tanzania Dk Mohammed Gharib Bilal amesema
tabia inayoendelea ndani ya bunge maalum la katiba inaweza kuleta hisia za
chuki na kuharibu mustakbali wa uundwaji wa katiba mpya.
Akifungua kongamano la
kuadhimisha miaka 50 ya Muungano mjini Zanzibar amesema ni vyema majadiliano ya
kujadili rasimu ya katiba yakazingatia kuleta maendeleo ya kiuchumi na kijamii
kwa miaka ijayo na si kuamsha hisia za kuwatenganisha wananchi.
Bilal amesema kundi lolote linalokosoa
muungano ni lazima kutumia njia za kujenga taifa na si kusababisha athari kubwa
kwa taifa
Amewataka wajumbe wa bunge hilo kuwacha
tabia ya kutoa maneno ya kashfa na badala yake kufanya kazi ya kutunga katiba
kwa maslahi ya watanzania.
Kongamano hilo la siku moja limewashirikisha
wakilishi kutoka taasisi za serekali ngos,wafanya biashra viongozi wa dini ,vyama vya siasa na wasomi
>>hapa>>
0 comments:
Post a Comment