April 21, 2014

Watanzania wametakiwa kutofautisha imani zao za kidini wakati wanapodai maslahi ya nchi ili iendelee kuwa na amani.
Akizungumza kwenye kongamano la miaka 50 ya katiba Mwenyekiti wa kongamano hilo Ali Saleh amesema  katika kipindi cha mageuzi ya katiba hakuna haja ya  kuibuliwa migongano ya kidini inayoweza kusababisha machafuko.
Amesema jambo la msingi la kujadiliwa ni vipi Zanzibar itakavyonufaika kiuchumi na kuongeza maendeleo baada ya katiba mpya na muundo wa serikali utakaokubalika.
Kongamano hilo lililoandaliwa na jumuiya ya Maimamu Zanzibar JUMAZA lililofanyika katika ukumbi wa Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar SUZA ambapo washiriki  wamewashauri  wanasiasa kuepusha kauli za kibaguzi, uchochezi na ukabila katika mchakato mzima wa kujadili rasimu ya pili ya katiba.
 

0 comments:

Post a Comment