April 20, 2014

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amesema maradhi ya Kisukari na Shindikizo la Damu ni tishio la vifo vingi Zanzibar na yamesababisha matatizo mengi ya Kiuchumi na Kijamii
Amesema pia yamezifanya familia nyingi Taifa na Dunia kubeba mzigo kutokana na gharama za matibabu yake.
Ameeleza kuwa Takwimu za mwaka 2012 za Shirika la Afya Ulimwenguni  WHO   zinaonyesha zaidi ya watu Milioni 4.8 wamepoteza maisha na Dola za Kimarekani zaidi ya Bilioni 471 zimetumika kupambana na janga la maradhi yasiyoambukiza.
Balozi Seif amefahamisha kwa hapa Zanzibar utafiti umeonyesha  asilimia 33% ya Wananchi wa  wanasumbuliwa na tatizo la shinikizo la Damu na asilimia 3.7% wanakabiliwa na  na maradhi ya Kisukari.
Amesema hayo katika ufunguzi wa Kampeni ya kutoa huduma za Shindikizo la Damu na Kisukari Zanzibar zinazoendeshwa na  Jumuiya ya Chuo cha Udaktari Tanzania -TAMSA mjini Zanzibar .
Amefahamisha kuwa  inakadiriwa ifikapo mwaka 2030 zaidi ya Dola za Kimarekani Bilioni 500 zinatarajiwa kutumika katika kupambana na na maradhi ya Kisukari na Shinikizo la Damu duniani kote.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar amesema kiwango hicho cha fedha ni kikubwa iwapo jamii itafanikiwa  kujiepusha na vishawishi vya kupata maradhi hayo Mataifa yanaweza kuzitumia katika masuala mbali mbali za maendeleo.
Ameongeza kuwa ili mwandamu ajiepushe na maradhi ya kisukari na shinikizo la damu njia pekee ya kujiepusha na maradhi hayo ni pamoja na kula mlo kamili kujiepusha na uvutaji sigara na unywaji wa pombe kiholela, tabia ya uvivu na ongezeko la uzito hatua itakayozuia kasi ya maradhi hayo Zanzibar kwa zaidi ya asilimia 80%.
Akitoa salamu katika uzinduzi wa zoezi hilo la upimaji afya Mkuu wa Chuo cha Kimataifa cha Udaktari Tanzania  IMTU Pro Flora Fabia Mbatia amesema mradi huo ni wa kwanza  Tanzania unalenga kuongeza ufahamu wa Taaluma ya kujikinga na maradhi yasiyoambukiza kwa wananchi.
Nae Mwenyekiti wa Chama cha Wanafunzi wa Udaktari Tanzania  TAMSA  amesema  utoaji wa huduma hizo za  afya, elimu pamoja na Dawa kwa wagonjwa wanaosumbuliwa na Maradhi ya Shinikizo la Damu na Kisukari utafanyika katika mikoa yote Zanzibar.
Balozi Seif Ali Iddi alilazimika kuzifungua sherehe hizo katika Ukumbi  wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar Kampasi ya Taasisi ya Kiswahili na Lugha za Kigeni  zilizopangwa kufanyika katika uwanja wa michezo wa Maisara Suleiman Mjini Zanzibar kufuaita amri ya Jeshi la Polisi Tanzania kuzuia mikusanyiko ya aina yoyote kwenye maeneo ya wazi katika kipindi hichi.


Naibu Waziri wa Afya Zanzibar Dokta Sira Ubwa Mamboya akimkaribisha Makamu wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Iddi katika uzinduzi wa kampeni za kutoa huduma za kisukari na shindikizo la damu zitakazofanyika Mikoa yote ya Zanzibar.



Makamu wa Pili wa Rais Balozi. Seif Ali Iddi akiwahutubia Madaktari na wananchi waliofika katika uzinduzi wa kampeni za kutoa huduma za kisukari na shindikizo la damu huko ukumbi wa Chuo Kikuu cha Taifa Suza Mjini Zanzibar.




Mkuu wa CHUO cha (IMTU) Prof. Flora Fabian akitoa maelezo kuhusu madaktari hao walivyojipanga kufanya kazi katika Mikoa yote ya Unguja na Pemba


Mratibu wa mtadi wa kutoa huduma za kisukari na shindikizo la damu Mr. Siraji M. Mtulia akitoa maelezo mafupi ya mradi huo utakaoanza kutekelezwa leo na Chama cha wanafunzi Madaktari Tanzania wakishikiana na Wizara ya Afya Zanzibar.





(PICHA ZOTE NA MAKAME MSHENGA WA MAELEZO ZANZIBAR).

0 comments:

Post a Comment