April 19, 2016



Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Dkt. Ali Mohamed Shein amefanya uteuzi wa viongozi katika Wizara mbali mbali za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kama ifuatavyo:
1. OFISI YA RAIS NA MWEYEKITI WA BARAZA LA MAPINDUZI
I. Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi – Dkt. Abdulhamid Y. Mzee
II. Katibu Mkuu – Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi – Nd. Salum Maulid Salum
III. Naibu Katibu wa Baraza la Mapinduzi – Nd. Salmin Amour Abdulla
2. OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA, SERIKALI ZA MITAA NA IDARA MAALUM ZA SMZ
I. Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ – Nd. Radhia Rashid Haroub
II. Naibu Katibu Mkuu, Ofis ya Rais, Tawala za Mikoa , Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ – Nd. Kai Bushir Mbarouk
3. OFIS YA RAIS, KATIBA, SHERIA, UTUMISHI WA UMMA NA UTAWALA BORA
I. Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi wa Umma na Utawala Bora – Nd. Asha Ali Abdulla
II. Naibu Katibu Mkuu, Ofis ya Rais, Katiba Sheria, Utumishi wa Umma na Utawala Bora anaeshughulikia masuala ya Utumishi wa Umma – Nd. Yakout Hassan Yakout
III. Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi wa Umma na Utawala Bora anaeshughulikia masuala ya Katiba, Sheria na Utawla Bora – Nd. Kubingwa Mashaka Simba.
4. OFISI YA MAKAMU WA PILI WA RAIS
i. Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais – Nd. Joseph Abdulla Meza
ii. Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Nd. Ahmed Kassim Haji
5. WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO
I. Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango – Nd. Khamis Mussa Omar
II. Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango – Nd. Ali Khamis Juma.
6. WIZARA YA BIASHARA, VIWANDA NA MASOKO
i. Katibu Mkuu wa Wizara ya Biashara, Viwanda na Masoko – Nd. Bakari Haji Bakari
7. WIZARA YA AFYA
I. Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya – Dkt. Juma Malik Akili
II. Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya – Nd. Halima Maulid Salum
III. Mkurugenzi Mkuu wa Wizara ya Afya – Dkt. Jamala Adam Taib
8. WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA AMALI
I. Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali – Nd. Khadija Bakari Juma
II. Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali anaeshughulikia masuala ya Mipango na Uendeshaji - Nd. Abdulla Mzee Abdulla
III. Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali –anaeshughulikia masuala ya Taaluma - Nd. Madina Mjaka Mwinyi
9. WIZARA YA ARDHI, MAJI, NISHATI NA MAZINGIRA
I. Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Maji, Nishati na Mazingira -  Nd. Ali Khalil Mirza.
10. WIZARA YA KILIMO, MALIASILI, MIFUGO NA UVUVI
I. Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi – Nd.Juma Ali Juma
II. Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi – Nd. Maryam Juma Abdulla
11. WIZARA YA KAZI, UWEZESHAJI, WAZEE, VIJANA, WANAWAKE NA WATOTO
I. Katibu Mkuu wa Wizara ya Kazi, Uwezeshaji, Wazee, Vijana, Wanawake na Watoto – Nd. Fatma Gharib Bilal
II. Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Kazi, Uwezeshaji, Wazee, Vijana, Wanawake na Watoto – Nd. Maua Makame Rajab
12. WIZARA YA HABARI, UTALII, UTAMADUNI NA MICHEZO
I. Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utalii, Utamaduni na Michezo – Nd. Omar Hassan Omar
II. Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utalii, Utamaduni na Michezo – Dkt. Amina Ameir Issa
13. WIZARA UJENZI, MAWASILIANO NA USAFIRISHAJI
I. Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji - Nd. Mustafa Aboud Jumbe
II. Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji- Nd. Shomari Omar Shomari
Uteuzi huo umeanza tarehe 18 Aprili 2016.Viongozi wote hao waliotajwa wanatakiwa wafike Ikulu kesho saa 8:30 za mchana tayari kwa kuapishwa.

0 comments:

Post a Comment