April 18, 2016

Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amezindua rasmi mbio za Mwenge wa Uhuru kwenye Uwanja wa Jamhuri Mkoani Morogoro leo.
Katika uzinduzi huo amesema utumbuaji majipu unalenga kuleta matumaini kwa wananchi ambao wamekata tamaa na kuleta heshima kwa wananchi waliodharauliwa.
Amemnukuu  Baba wa Taifa Mwl Julius Nyerere akisema kuwa nia ya Mwenge wa Uhuru tangu mwanzo ni kumulika mipaka ya nchi yetu dhidi ya maadui, kuleta matumaini pale ambapo hakuna matumaini, kuondoa chuki pale ambapo kuna chuki na kuleta heshima pale ambapo kuna dharau.
Hhivyo dhana ya Mwenge huo inaendana na dhana ya kutumbua majipu katika Serikali ya awamu ya tano.
“Kaulimbiu ya mbio ya za mwenge mwaka huu ni hii: Vijana ni nguvu kazi ya taifa, washirikishwe na wawezeshwe,”
 Amezitaja baadhi ya sababu au changamoto zinazowakabili vijana nchini kuwa ni ukosefu wa ajira, uwezo mdogo wa kuajiri, ukosefu wa mitaji rafiki kwa vijana, maeneo ya kufanyia kazi pamoja na mitazamo hasi kwa baadhi ya vijana katika kuchagua kazi.
Makamu wa Rais pia amewataadharisha vijana juu ya ongezeko la kubwa la maambukizi ya ukimwi na matumizi ya madawa ya kulevya na kueleza kuwa matatizo hayo pia zinaongeza mzigo kwa jamii na serikali katika kuwatibu, kuwahudumia na kuongezeka kwa vifo.
Kwa upande wake, Waziri Nchi katika Ofisi ya Waziri Mkuu Jenista Mhagama, amemtambulisha George Jackson Kijimba kuwa ndiye kiongozi wa mbio za mwenge mwaka huu akisaidiana na wakimbiza mwenge  wengine watano na ukimbizaji mwenge huo wa uhuru zitaishia  mkoani Simiyu tarehe 14 Oktoba mwaka huu.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mhe. Samia Suluhu Hassan, akihutubia Taifa kwenye Sherehe za
uzinduzi wa Mwenge wa Uhuru kitaifa zilizofanyika leo
April 18, 2016 katika Uwanja wa Jamhuri Mkoani Morogoro.

0 comments:

Post a Comment