April 21, 2016



Jumuiya kimataifa ya Intanational Holly of Quran Memorazation yenye makao yake nchini Saudi Arabia inatarajia kufungua chuo cha kuhifadhia Qurani Kisiwani Pemba hivi karibuni ilikuendeleza watoto wakislamu kujifunza kuhifadhi qurani  kwa wingi visiwani humo..
Akizungumza na mwandishi wa habari hii Kisiwani Pemba Mjumbe wa tasisi hiyo Abdul Azizi al-Umiry amesema madrsa hiyo  tayari imeanza kujengwa  na inatarajia kumalizika hivi karibuni
Amesema ujio wao kisiwani pemba ni kutoa mafunzo kwa walimu wa madrasa na wanafunzi walio kwisha hifadhi Quran juzuu 30 ili kutafuta mbinu bora za kuwafundisha wanafunzi njia itakayo kuwa nyepesi kwao kuhifadhi kitabu kitukufu cha Qur an
Akizungumza wakati wa kufungua mafunzio hayo mbunge wajimbo la Mgogoni DR Suleiman Ali Yusufu amesema ujio wa huo ujumbe ni jitihada zinazo endelea kufanywa na jumuiya ya kuhifadhi Quran kisiwani humo ili kufanikisha maendekleo ya kuhifahi qurani kisiwani pemba
Ujumbe huo unatarajiwa kuwepo Pemba kwa siku mbili na utaendelea na mafunzo kama hayo huko Unguja

0 comments:

Post a Comment