Wananchi wa Zanzibar wanashiriki katika Uchaguzi wa
marudio ambapo rais wa Zanzibar baada ya matokeo ya uchaguzi uliofanyika 25
Oktoba mwaka jana kufutwa na tume ya uchaguzi.
Uchaguzi huo wa marejeo unaosimamiwa na Tume
ya Uchaguzi Zanzibar {ZEC} umetoa nafasi kwa Wananchi wa Zanzibar
kukamilisha kupiga kura kwa nafasi Tano ikiwemo Rais wa Zanzibar Mwakilishi,
Diwani.
Mgombea urais wa Chama cha Mapinduzi (CCM) visiwani Zanzibar Dkt
Ali Mohammed Shein amepiga kura katika yake katika kituo cha Bungi, Kibele wilaya ya kusini Unguja.
Akizungumza na wanahabari
baada ya kupiga kura amesema anaamini kuwa uchaguzi huo utakuwa huru na amani.
Mgombea urais wa chama cha ADC Hamad Rashid
amepiga kura yake kituo cha Tondooni Wawi wilaya ya Chake-Chake mkoa wa Kusini
Pemba na amesema ana imani ya kuwa Rais au
kuwa Makamu wa Rais wa Zanzibar.
Nae Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif
Ali Iddi na Mkewe Mama Asha Suleiman Iddi wamepiga
kura katika Kituo chao cha Skuli ya Sekondari ya Kitope Jimbo la Mahonda Mkoa
wa Kaskazini Unguja mnamo saa 2.4 za asubuhi.
Balozi Seif anagombea nafasi ya Ujumbe wa
Baraza la Wawakilishi Zanzibar kupitia CCM katika Jimbo jipya la Mahonda badala ya
lililokuwa Jimbo la Kitope.
Akizungumza na waandishi wa Habari mara baada ya
kupiga kura Balozi Seif amesema ameridhika na zoezi zima liloanza mapema
asubuhi na wananchi mbali mbali wameshatumia haki yao ya kupiga kura na kurejea
nyumbani kuendelea na shughuli zao za kimaisha.
Balozi Seif anagombea nafasi ya Ujumbe wa
Baraza la Wawakilishi Zanzibar kupitia CCM katika Jimbo jipya la Mahonda badala ya
lililokuwa Jimbo la Kitope.
Chama cha Wananchi (CUF) hakijashirikia uchaguzi huo kikiamini kuwa
kilishinda katika uchaguzi ule wa Oktoba
25 mwaka jana.
0 comments:
Post a Comment