Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli, na Rais wa Zanzibar Dkt Ali Mohamed Shein wamemtembelea Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad
katika holeti ya Serena Jijini Dar es Salaam. Maalim Seif yupo hotelini hapo
kwa mapumziko baada ya kutolewa hospitali ya Hindu Mandal jana jioni alipokuwa
amelazwa.
Maalim Seif amewahakikishia Watanzania kuwa afya yake inaendelea
vizuri na kwamba anaendelea na shughuli zake na siku chache zijazo ana
matumaini ya kurejea katika hali yake ya kawaida.
0 comments:
Post a Comment