Makamu wa
Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amewaagiza watendaji wa
Wizara ya Afya hasa Madaktari na wauguzi kuhakikisha kwamba dhima
waliokabidhiwa na jamii katika kuwahudumia Wananchi Kiafya
wanaitekeleza kwa moyo na imani kama walivyokula kiapo.
Balozi Seif
alisema Madaktari na wauguzi wanapaswa kutambua kwamba wao ndio dhamana wa kulinda afya za
Wananchi katika maeneo yao, kinyume cha wajibu huo watarajie kujenga chuki na
uhasama kati yao na Wananchi hao hasa wagonjwa wanaopelekwa kuwahudumia.
Makamu wa
Pili wa Rais wa Zanzibar aliwatahadharisha baadhi ya Madaktari na wauguzi wenye hulka ya
kunyanyasa wagonjwa kwa kisingizio cha itikadi za Kisiasa waelewe kwamba
tabia hiyo hawaikomoi Serikali bali wanawatesa Wananchi hasa wagonjwa wasiokuwa
na hatia yoyote.
Akizungumzia
tatizo laTanuri la kuchomea taka taka za Hospitali hiyo ya Chake chake Pemba Balozi Seif
aliulaumu Uongozi wa Wizara ya Afya kwa kushindwa kukamilisha ujenzi wa Tanuri
hilo kwa miaka Mitano sasa.
Alisema hali
hiyo haileti sura nzuri katika dhana nzima ya uwajibikaji kwa watendaji hao jambo ambalo
Serikali Kuu italazimika kulichukulia hatua za haraka tatizo hilo lenye kuleta
hali ya wasi wasi wa afya za Wananchi wanaoishi karibu na maeneo hayo.
Balozi Seif
aliuonywa Uongozi wa Wizara ya Afya kwamba kama utashindwa uwezo wa kutoa shilingi
Milioni 3,500,000/- hata kwenye O.C
za mwezi za Wizara hiyo kujenga Tanuri jengine basi ataamua kutoa fedha yeye
mwenyewe kuondosha kadhia hiyo inayoleta kero na wasi wasi kwa wakaazi wa
maeneo ya Mji huo.
Bibi Hanun
alisema Wananchi hao wamekuwa wakishuhudia baadhi yawanyama kama Mbwa na Paka
wakiranda na taka taka hizo ambazo nyengine ni za hatari na zinaweza
kusababisha kutapakaa kwa maradhi ya kuambukiza.
Balozi Seif akikagua baadhi ya wagonjwa kwenye wodi tofauti za
Hospitali ya Chake chake Pemba akiongozwa na
Muuguzi wa Wodi ya Akina mama bi Hassanat Abdalla.
|
Balozi Seif akikagua Tanuri la kuchomea taka
taka za Hospitali ya
Chake chake ambalo limeshindwa
kutoa huduma tokea
lilipojengwa kwa miaka mitano sasa
|
0 comments:
Post a Comment