Jumla ya tani 4,711 za karafuu kavu zenye
thamani ya shilingi bilioni 66 zimenunuliwa na Shirika la Biashara la Taifa
Zanzibar ( ZSTC) kisiwani Pemba, tangu kuanza kwa msimu wa karafuu
hadi kufikia mwanzoni mwa mwezi huu wa January.
Afisa mdhamini wa ZSTC Abdalla Ali
Ussi, amesema shirika hilo limejipanga kununuwa karafuu zote bila ya kumkopa wakulima
hata mmoja sambamba na kuwalipa fidia wachumaji wa zao hilo watakaopata hasara
ya kuanguka mikarafuu kwa bahati mbaya.
Nae Mkurugenzi fedha wa shirika hilo Ismail Khamis
Bhai amesema kwa mwaka 2015/2016 limetowa mkopo kwa wakulima wa
karufuu Zanzibar wa zaidi ya shilingi milioni 342.
0 comments:
Post a Comment