Kiasi ya shilingi
bilioni 5 zimetengwa kwa ajili ya utanuzi wa barabra ya Mwanakwerekwe
makubaburini hadi Fuoni kituo cha polisi
yenye urefu wa kilomita 4.
Barabara hiyo
itajengwa na Idara ya ujenzi na utunzaji wa barabara Zanzibar UUB na fedha hizo
ni makusanyo ya kodi za wananchi kupitia vyanzo mbalimbali vya mapato.
Mhandisi Mkuu wa
utunzaji wa barabara Zanzibar Cosmas Masolwa amesema kwa sasa idara imenza kazi
ya kutanua upana wa barabara na baadhi ya nyumba zitavunjwa.
Hata hivyo
ameeleza kwa wananchi wanaovunja au kuvunjiwa nyumba hizo hawataliwa fidia
yeyote kwa kuwa walikiuka masharti ya ujenzi na kuvamia hifadhi ya barabara.
Mhandisi Msolwa
amesema idara taarifa zilikuwa zinatolewa kwa wananchi waliokuwa wanajenga
ndani ya hifadhi ya barabara lakini wengi yao walikaidi amri hiyo.
Amefahamisha
kuwa barabara hiyo ilikuwa inaharibika mara kwa mara hivyo imelazimika
kufanyiwa matengenezo kutokana na uchakavu uliozidi.
Mbali na mradi
huo pia inaendelea na miradi mengine ya barabara inayojengwa kwa kiwango cha
lami ukiwemo ule wa barabara ya Bungi muembe kiwete wa kilimoita 2.2, Chuo cha utalii ndani wenye
urefu wa mita 400 na wa Chuo cha Fedha Chwaka wa kilomita moja na mengine iko Pemba.
0 comments:
Post a Comment