Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein amewataka wananchi kuamini kuwa Serikali ipo na
inaendelea na kazi za kuwahudumia wananchi.
Amesema hayo alipotembelea
mradi wa maji huko Makunduchi Mkoa wa Kusini Unguja.
Amesema utekelezaji wa mradi huo ni miongoni mwa kazi inazofanya ili kuwapatia huduma ya uhakika ya maji safi katika kipindi kifupi kijacho.
Amesema utekelezaji wa mradi huo ni miongoni mwa kazi inazofanya ili kuwapatia huduma ya uhakika ya maji safi katika kipindi kifupi kijacho.
Dk. Shein amesema
visima vitatu vimechimbwa vitapeleka maji katika tangi hilo kubwa
lililobadilishwa kupitia mradi wa Ras el Khaimah ili kusambaza maji ya kutosha kwa matumizi ya wananchi.
Waziri wa Ardhi, Makaazi, Maji na Nishati Mhe.
Ramadhan Abdalla Shaaban amebainisha kuwa kazi ya ulazaji wa mabomba kutoka
kisima kipya cha pango la Mnywambiji huko Kibuteni iko mbioni na imebakia sehemu
ndogo kukamilika.
Mradi huo wa ubadilishaji wa tangi pamoja na uchimbaji wa kisima kipya huko makunduchi unatekelezwa
kwa ushirikiano wa SMZ, Uongozi wa Jimbo, Taasisi ya Milele Zanzibar Foundation
pamoja na wananchi.
0 comments:
Post a Comment