November 24, 2015


Waziri Mkuu wa Tanzania Majaliwa Kassim Majaliwa ameitaka wizara ya Tawala  za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI  kujieleza ni sababu ya kuchelewa hadi sasa kuanza kazi mradi wa mabasi yaendayo kasi DART.
Amesema anashangazwa na mradi huo katika taarifa zinaonyesha kuwa umekamilika lakini hadi sasa hajaanza kazi na hajui kinachokwamisha hilo.
Waziri mkuu ameagiza watendaji wote wa wizara ya TAMISEMI, akiwemo Katibu Mkuu wa Wizara hiyo kufika Ofisini kwake kesho asubuhi kueleza kuchelewa mradi huo wakati miundombinu imeshakamilika.
Ameyasema hayo alipotembelea Wizara ya TAMISEMI na kuongea na watendaji wa wizara hiyo huku akiwataka watendaji kufanya kazi kwa mujibu wa hotuba ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli aliyoitoa Bungeni hivi karibuni.
Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kikao hicho Katibu Mkuu wa TAMISEMI Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Jumanne Sagini amewaagiza watumishi katika wizara hiyo kufanya kazi kwa bidii kwa kuzingatia maadili pamoja na kujiepusha na tabia ya uzembe, uvivu na wizi katika maeneo yao ya kazi.





0 comments:

Post a Comment