November 25, 2015



Bodi ya Chakula, Dawa na Vipodozi imekamata vipodozi vilivyopigwa marufuku kuingizwa nchini katika Bandari Kuu ya Malindi Zanzibar.
Vipodozi hivyo ni pamoja na Movet Crèame kutoka nchini Italia na Medical Fade Crème kutoka Marekani vyenye uzito wa tani tatu vilikuwa yamechanganyishwa na vitu vingine katika Makontena bandarini hapo.
Akitoa taarifa kwa waandishi wa habari Mkaguzi wa Bodi hiyo Nassir Buheti amesema vipodozi hivyo vimepigwa marufuku kutokana na kuwa Viambata vyenye kemikali vinavyoweza kuleta madhara Mtumiaji ikiwemo ugonjwa wa saratani, Ulemavu pamoja na uharibifu wa ngozi.

Amefahamisha kuwa mawakala wa vipodozi hivyo wamedai kuwa  havikukusudiwa kuingizwa nchini wakati vimepigwa marufuku dunia nzima.
Mkaguzi Buheti amesema sheria ya Chakula, Dawa na Vipodozi ya mwaka 2006 inasema si ruhusa kuingiza, kuuza, kusambaza vipodozi haramu na kuwataka wafanyabiasha wa vipodozi, dawa pamoja na Chakula kutofanya udanganyifu wa bidhaa wanazoingiza ili kuepuka madhara yasiongezeke nchini.

Baadhi ya Vipozi vyenye Kemikali vilivyopigwa marufuku kutumika duniani vikiwa vimetolewa katika Maboxi yaliyotumika kuviihifadhi. Vipodizi hivyo Vinasubiri kuteteketezwa na Maafisa wa Bodi ya Chakula, Dawa na Vipodozi Zanzibar.



Maelezo Zanzibar

0 comments:

Post a Comment