Jumuiya ya Umoja wa ulaya -EU unakusudia kuziendeleza taasisi za kiraia nchini kupitia mradi wa uimarishaji wa sera na miongozo yao ya kiutendaji unaogharimu shilingi bilioni 6.82.
Mradi huo wa miaka mitano utazisaidia taasisi hizo katika masuala ya uongozi, mafunzo, kupunguza umasikini pamoja na kuzuwia ajira za watoto Zanzibar.
Balozi maalum wa jumuiya ya ulaya Filiberto Ceriani akizungumza katika hafla ya utiaji saini mpango huo amesema EU imelenga kuziwezesha taasisi hizo za kiraia kufanya kazi zake kwa ufanisi na kuimarisha utawala bora .
Mwenyekiti wa mtandao wa jumuiya za kiraia Zanzibar -ANGOZA Asha Aboud amesema taasisi hizo zimekuwa zikifanya kazi kwa mazingira magumu yanayosababisha kushidwa kufikia malengo.
0 comments:
Post a Comment