May 08, 2014

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amewataka Majaji wanawake kushirikiana zaidi katika kutoa haki sawa kwa mshitakiwa na aliyedhalilishwa  wanaposhughulikia kesi mbali mbali hasa  za udhalilishaji wa kijinsia.
amefahamisha kuwa unyanyasaji huo kwa  kiasi kikubwa unawaandama zaidi wanawake na watoto katika Mataifa mbali mbali duniani hasa katika nchi changa.
"Wasimamizi wa sheria kwa kushirikiana na wananchi wanapaswa kushirikiana katika kupiga vita vitendo hivyo viovu." amesema Balozi Seif
akifunga  Mkutano wa  Kimataifa wa Chama cha Majaji Wanawake Duniani {IAWJ }  huko Arusha  Balozi Seif amesema  Majaji Wanawake wana wajibu wa kuvitumia vyombo vya Habari katika kutoa elimu kwa umma itakayosaidia kupunguza wimbi huilo la unyanyasaji wa kijinsia ndani ya Jamii.
amemeleza kuwa uelewa mkubwa miongoni mwa Jamii ndio msingi imara na sahihi unaochangia kupunguza matatizo makubwa yanayowakabili wananchi.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar   amesema mkutabo huo kwa kiasi kikubwa umetoa fursa ya kupanua wigo wa mawasiliano kati ya Majaji Wanawake Duniani ili kujenga mazingira bora ya uwajibikaji.
 Mwenyekiti wa Chama cha Majaji Wanawake Duniani Jaji Eusebia Munuo aMEsema Wanachama wa Chama hicho wanshirikiana na taasisi na vyama vyengine katika kusimamia upatikanaji wa haki,  elimu ya haki za binaadamu na jinsi huduma za mahkama kwa wanawake

0 comments:

Post a Comment