April 03, 2014

WIZARA ya Afya kupitia Kitengo Cha Maradhi yasioambukiza Zanzibar inafanya utafiti wa kupata uelewa wa jamii  kuhusiana na maradhi ya Kisukari, shinikizo la damu na saratani.
Utafiti huo utafanyika katika  Wilaya  ya Kaskazini A, Wilaya ya Mjini,  Magharib kwa Unguja na Micheweni na Chakechake na wananchi 712  watahojiwa.
Meneja wa Kitengo cha Maradhi yasiambukiza Zanzibar Omar Mwalim Omar amesema kuwa lengo la utafiti huo ni kuelewa ufahamu wao, imani, na desturi kuhusu maradhi yasioambukiza.
 Akizungumzia hali halisi ya maradhi yasioambukiza Zanzibar amesema    yanaendelea kuathiri jamii na ameiomba Serikali na washirika wa maendeleo kuelekezea nguvu zao kwa pamoja  kupambana na maradhi hayo.
Maradhi yasiambukiza yanaongoza Zanzibar ni kisukari, saratani ya matiti, shingo ya kizazi na saratani ya kibofu cha mkojo kwa wanaume na kwa sasa maradhi hayo mengi yao hayana takwimu sahihi.
Amesema  ameimba Serikali na washirika mbali mbali wa maendeleo kuelekezea nguvu zao kwa pamoja katika kupambana na maradhi hayo ambayo yanathiri jamii kwa kiasi kikubwa.

0 comments:

Post a Comment