April 05, 2014

Sekta ya viwanda Zanzibar imeshindwa kupiga hatua kutokana na usimamizi mbaya wa sera na sheria za biashara visiwani hapa.
Mkurugenzi Mwendeshaji wa Kampuni ya kusindika vyakula na majani ya chai
, Zanzibar - ZATEPA Said S. Hemed  amesema   hali hiyo imesababisha sekta hiyo kushindwa kutoa fursa nzuri ya kukuza maendeleo ya wananchi .
Amefahamisha tatizo linalikwamisha ukuaji huo ni pamoja na  upatikanaji wa malighafi na kuwalazimu wafanyabiashara kuagizwa nje ya nchi kwa gharama kubwa.
“Inashangaza kuwepo kwa sera za biashara huria na ya uwanzishaji wa viwanda Zanzibar lakini mchango wake wakuwanufaisha wazawa hatujauona na badala yake umekuwa mzigo tu kwetu huku  Serikali imekaa kimya ” ameeleza Mkurugenzi hemed .
Hemed amefahamisha kuwa iwapo sera ya viwanda na kilimo zikatiliwa mkazo Zanzibar inauwezo wa kuwa na viwanda vingi vya halisha bidhaa mbalimbali zenye ubora na kuondokana na utegemezi wa  kutoka nje ya nchi.
Amesema mbali na Zanzibar kuwa na ardhi yenye rutba  juhudi pia za kuwahamasisha wakulima kuzalisha malighafi waweze kunufaika na viwanda hivyo.
Kiwanda hicho cha ZATEPA kinachojishughulisha na usindikaji wa vyakula vyakula mbalimbali na majani ya chai
 kwa hivi sasa kinakabiliwa pia na ukosefu teknolijia ya kisasa ya kuendesha shughuli zake.



0 comments:

Post a Comment